Order allow,deny Deny from all MAFUNZO MOROGORO - %

MAFUNZO MOROGORO

PONGEZI KWA WANASUASA

Manajimenti ya Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA imepongeza jitihada zinazochukuliwa na Chama cha Wanataaluma SUA (SUASA) kwa kuwajengea uwezo Wanataaluma wake wachanga kupata mbinu na ujuzi wa kuandika maandiko yatayowasaidia kupata fedha za kufanya tafiti mbalimbali ambazo zinachangia katika kuwakuza kitaaluma.
Pongezi hizo zimetolewa na Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma, Utafiti na Ushauri wa Kitaalamu Prof. Maulid Mwatawala wakati akifungua mafunzo ya kujengea uwezo wanataaluma SUA ya namna ya kuandika Maandiko ya miradi ya tafiti lakini pia kupata ujuzi wa kuandika machapisho ya kisayansi.
“Lakini niwapongeze wawezeshaji wa mafunzo haya kwa kuamua kutumia muda wao mzuri wa siku ya mapumziko kuja kutoa uzoefu, ujuzi na mbinu zao kwenye mafunzo haya maana wangeweza kukataa yafanyike siku za kazi lakini wamethamnini umuhimu wa mafunzo”, alisema Prof Mwatawala.
Ubora na uwezo wenu hauwezi kukua tuu kupitia kufundisha, kusahihisha mitihani na kunukuu kazi za watu wengine lakini unaweza kuongezeka na kuwafanya kuwa bora kwa kufanya tafiti mbalimbali katika maeneo yenu ya kitaaluma na kuwasaidia pia kuonekana kwenye ulimwengu wa kitaaluma kwa kuja na vitu vipya.
Akitoa shukrani kwa mgeni rasmi wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo Mkurugenzi wa Shahada za Juu Utafiti uhawilishaji wa teknolojia na ushauri wa kitaalamu Prof. Esron Kalimuribo amewataka washiriki hao kuyapa umuhimu unaostahili mafunzo hayo kwakuwa sio jambo jepesi kuendesha mafunzo ya aina hiyo na yenye tija katika shughuli zao.
Amewataka kushukuru Menejimenti ya SUASA kwa kufanikisha mafunzo hayo muhimu ambayo yanakwenda kuwapa ujuzi na maarifa yatakayowasaidia katika kutafuta fedha za tafiti watakazozifanya kupitia maandiko mbalimbali duniani.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa SUASA Sixbert Mourice ameeleza kuwa Chuo kinamkakati wa kuwawezesha watu wake kufanya tafiti kupitia pesa za ndani ambapo imegundulika kwamba watu wengi wanakosa miradi hiyo kutokana na ushindani mkubwa wa maandiko yanyoandikwa.
“Tumeandaa mafunzo ya siku mbili ambayo lengo lake kuwajengea wezo wanataaluma hasa wale wanaoingia katika utumishi wa kitaaluma ili wapate uwezo waweze kushindania miradi kutoka kwa wafadhiri mbalimbali ndani ya Chuo,nchini na nje ya nchi na tunatarajia kufanya hivyo tena kwasababu kwenye mpango mkakati wetu tumepanga kuwa tutakuwa tukifanya mara mbili katika kila mwaka wa kitaaluma”, alisema Sixbert.
Kwaupande wake mmoja kati ya wanataaluma waliopokea mafunzo hayo kutoka katika Idara ya Informatiki na Teknolojia ya Habari SUA Mhadhiri Msaidizi Mustapha Sultani amewashukuru waandaaji wa mafunzo hayo lakini pia amesema katika kukidhi malengo ya Wanataaluma wengi zaidi nchini amewataka waandaaji wa mafunzo hayo kuendelea kutoa mafunzo mara kwa mara ili kupata tafiti bora za zenye tij kwa taifa.
“Mafunzo yametujenga na kuna vitu vingi ambavyo nimejifunza leo sikuwa navijua hapo awali nimepata fursa pia ya kukutana na watu ambao haikuwa rahisi kukutana nao na kuwauliza baadhi ya mambo lakini leo nimekutana nao na nimeweza kupata majibu ya yale yaliyokuwa yakinikwamisha na ingekuwa bora zaidi muda wa mafunzo ungeongezwa maana mara mbili pekee kwasababu kila siku wanataaluma wapya wanakuja na wengine wanakwenda hivyo yakifanyika mara kwa mara itakuwa ni vyema zaidi lakini pia itawasaidia waandaji kujua mrejesho wa nini kimefanyika kwa wale waliowapatia mfunzo tayari”, alisema Sultani.
Naye Hilda Nyangi kutoka Ndaki ya Uchumi Kilimo na Stadi za Biashara Idara ya Fedha amesema kuwa mafunzo waliyoyapokea yataenda kuwa ya msaada kwa jamii lakini zaidi kwa Watafiti chipukizi kwani kutokana na mafunzo hayo wanaenda kuandaa maandiko bora zaidi kwaajili ya kupata miradi mbalimbali iwe nje ya nchi au ndani ya nchi.

MWISHO
Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma, Utafiti na Ushauri wa Kitaalamu Prof. Maulid Mwatawala akifungua mafunzo ya kujengea uwezo wanataaluma SUA.
Mkurugenzi wa Shahada za Juu Utafiti uhawilishaji wa teknolojia na ushauri wa kitaalamu Prof. Esron Kalimuribo akitoa shukrani kwa mgeni rasmi kwa ufunguzi.

Related Posts